1. EMMANUEL MBOGO: Vipuli vya Figo

Chacha alimsindikiza Alice kwa macho ya uchu akimmezea mate. ‘Afadhali nioe kuliko kuendelea na ukapera huu,’ fikira zilimpita kichwani mwake, zikayeyuka hewani. Katika suala hili la kuoa, Chacha alikatishwa tama na utamaduni wa kwao uliomtaka mwoaji alipe mahari ng’ombe chungu nzima kabla ya kumpata mke. Uwezo kama huo hakuwa nao yeye wala wazazi wake. Lakini Licha ya hayo yote bado wazazi wake walisisitiza kuwa akitaka kuoa lazima arudi atafute mchumba wakabila lake. ‘Wacha tu; mimi dawa ya wazee wale naijua,’ aliwaza. ‘Nitaoa motto mzuri wa humu humu jijini, nizae naye motto mmoja au wawili kasha nifunge safarikwenda nyumbani. Hakuna mzazi anayechukia wajukuu wake…’

Kule jikoni Alice aliinjika sufuria ya chai akaiacha ichemke. Kisha tena, katika figa jingine la jiko lile la umeme akabandika maji ya kuchemshia mayai.

“Habari za asubuhi?” aliamkua Angela.

Alice aligeuka akitabasamu na kujibu, “Nzuri, Angela. Mbona umeamka mapema leo?”

“Aa, sijui, sina usingizi,” alisema Angela na kukaa kwenye stuli pembeni kidogo karibu na friji. “Leo usingizi wangu haukuwa mzuri; naota ndoto mbaya mbaya tu.” Alipiga mwayo, “Mama kaamka?”

“Bado! alijibu Alice, “nimewasha umeme muda mrefu, nadhani maji yamepata moto, unaweza kwenda kuoga…”

Angela alisimana, “Hivi baba aliruda jana? Maana Sikulisikia gari lake.”

“Hata mimi sikulisikia.”

“Mlinzi anasemaje?”

“Anasemahakurudi.”

“Aa, baba naye bwana!” Alilamika Angela, bintiye Dkt Matoga aliyekuwa amerudi likizo toka Ughaibuni ambako alikuwa anasomea shahada ya pili katika utaalamu wa kompyuta. Huuulikuwa mwaka wake wa pili nab ado mwaka mmoja ulikuwa unamsubiri. Angela alikuwa motto wa pili wa Dkt. Matoga. Wa kwanza alikuwa mvulana – Bruno. Bruno, badda ya kumaliza mafunzo ya shahada ya uhandisi – umeme, alifanya kazi kwa muda pale jijini Daluta. Kisha tena kwa msaada wa hadhi ya babke Waziri wa Afya, Bruno alipandishwa cheo na sasa alikuwa huko jimbo la kaskazini kama Mhandisi Mkuu wa Mkoa huo. Bruno alikuwa tayari ameoa na ana watoto wawili – Janet na Rose.

Maswali:

a) Liweke dondoo hili katika muktadha wake

b) Jadili maudhui yanayodhihirika katika dondoo hili

ch) Fafanua mafunzo yanayopatikana katika dondoo.

d) Tambua na ueleze semi zilizotumiwa katika dondoo hili

e) Jadili jinsi Dkt Matoga anavyoathirika kutokana na sifa zake kama zinavyoelezwa katika dondoo.

 

2. AYI KWEI ARMAH: Wema Hawajazaliwa

Koomson alikuwa amekaa juu ya kitanda kilichoko nyuma ya pazia. Hajijui kwa hofu! Anaona kwamba kukitamkwa neon moja tubasi uhai wake umefikia siku yake ya mwisho. Alikuwa amevva suti ya sufi ambayo ni nyeusinyeusi, shati jeupe lililotakata weupe wake, na tai nyeusi. Juu ya pua yake kulikuwa na vitone vilivyoonyesha kama vitakavyokuwa vikubwa na kudondoka baada ya dakika chache tu. Lakini havikudondoka. Kwa dakika Fulani hivi, Koomson alikaa bila ya hata kutukuta; alitulia tuli kama mtu anayeiua kuwa ni muhimu sana kwake kutoteteleka hata kidogo. Koomson akayainua macho yake taratibu kama ambaye hataki aonekane na watuwasioonekana lakini walioko hapo hapo, kasha akamwangalila Yule bwana. Yule bwana hakuweza kuufahamu mtazamo wa Koomson kwa vile tabia ya Koosom ilikuwa imebadilika kabisa. Mara Koomson akawa anaashiria upesi upesi – mwanzo akaelekeza kidole kwenye taa, kasha akaielekeza kwenye dirisha lililo wazi. Hofu aliyonayo ikatokeza katika kila kiungo cha mwili wake.

Yule bwana akazifahamu hizo ishara. Akaizima taa. Kisha akasogea dirishani, akalifunga. Akamngojea Koomson aseme, lakini hakusema kitu isipokuwa pumzi zilikuwa zikimpanda na kumshuka, hofu zimemshika, tumbo linamnguruma, na mashuzi yanamtoka. Chumba kikawa hakikaliki. Macho yake yalipokwisha kulizoea giza, akayaona macho ya Koomson yanayong’aa kati ya uso wake mweusi. Macho yake Koomson yalikuwa bado yanaangalia upande liliko dirisha, ingawa kila asikiapo sauti yoyote alikuwa upesi akiangalia upande wa mlango. Baadaya muda, weupe wa shati la Koomson ulidhihirikatena.

Kuna wakati mmoja Yule bwana alimwona Koomson akiliangalia shati lake mwenyewe, kama hatari. Huko kumwona huyo mtu was Chama kuwa leo yuko hapo kwake, na akawa anaogopa kuwa kila dakika ipitayo itakuwa ndiyo ya mwisho wa maisha yake, kulimkumbusha Yule bwana ile siku yeye na Oyo walipokwenda nyumbani kwa Koomson. Akkifananisha siku ile siku ile na siku ya leo, Yule bwana akaona kuwa kuna tofauti kubwa hasa kule kujiamini alikokuwa nakp katika hizo siku zilizopita. Itakuwa ni makosa, tena makosa makubwa kufikiri kama alivyokuwa akifikiri kwamba haya mabadiliko hayawezi kuleta kitu chochote kipya katika maisjaya taifa lenyewe, labda hakuna kipya kitakachotukia. Hawa wapya walioshika serikali sasa, watayatumia madaraka yao kuiba mali ya nchi na kuyatumia kwa maslaha ya nafsi zao. Hilo, bila ya shaka, ndilo linalotarajiwa kuwa. Hawa wapya watayatumia madaraka ya nchi wawatese wale wanaume na wanawake wasiotuma lugha ya kuwadanganya hao wahika madaraka wapya. Hakutakuwa na tofauti yoyote. Hayo yatakuwa ni mfululizo wa mtindo wa maisha ya Ghana.

Maswali:

a) Liweke dondoo hili katika mutktadha wike

b) Eleza mabadiliko yanayotokea katia dondoo hili

ch) Changanua maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili.

d) Fafanua sifa zake Koomson vile zinanyodhihirika katika dondoo

e) Changanua mafunzo yanayopatikana katika dondoo.

 

MWENDA MBATAIAH : Msururu wa Usaliti

3.a) Ukitoa mifano katika riwaya, Msuru wa Usaliti, fafanua sababu zilizochangia uundaji wa chama cha upinzani cha Umoja wa Wazalendo wa Taifa (UWATA)

b) Eleza umuhimu wa vyama vya upinzani katika serikali za nchi zinazoendelea.

 

4. Kwa kutumia mifano mwafaka, fafannua vile mwandishi anavyomsawiri mwanamke katika riwaya, Msururu wa Usaliti

 

CHINUA ACHEBE: Mwakilishi wa Watu

5.a) Ukirejelea riwaya ya Mwakilishi wa Watu, fafanua madhara ya kisiasayaliyowaangukia viongozi wa chama cha upinzani cha Common People’s Convention (CPC) na Peoples’ Organisation Party (POP).

b) Vyama vya kisiasa katika jamii yako vinapata matatizo yaoi katika kutekeleza malengo yao?

 

6.a) “Mteni nanga anaonyesha mfano mbaya wa viongozi.” Thibitisha ukweli wa dai hili kwa kutoa mifano katika riwaya, Mwakilishi wa Watu

b) Ungekuwa mwanasiasa, ungefanya nini ili kuridhisha mahitaji ya watu wako?

 

SAID A MOHAMED: Dunia Yao

7. a) Eleza tabia za Mtima kama zinavyowasilishwa katika riwaya Dunia Yao na Said A. Mohamed.

b) Jadili jinsi familia ya Ndi inavyotengana

 

8. Jadili ufundi wa kisanii mwandishi anaotumia kwendeleza riwaya, Dunia Yao.

 

MUHAMED S. MOHAMED: Nyota ya Rehema

9. Ukirejelea riwaya, Nyota ya Rehema, jadili namna mwanamke alivyosawiriwa.

 

10. Tambua na ueleze mbinu za kisanaa msanii alizotumia kuwasilisha uiumbe wake katika riwaya, Nyota ya Rehema

 

SAID A. MOHAMED: Nyuso za Mwanmke

11. “Utamaduni ndiyo maudhini ya pekee katika riwaya, Nyuso zza mwanamke. Jadili.

 

12. Jadili sifa za wahusika wafuatao katika riwaya, Nyuso zza mwanamke na Said A. Mohamed

a) Nana

b) Faisal

 

KEN WALIBORA: Ndoto ya Almasi

13. a) Ukitumia mifano kutoka riwaya, Ndoto ya Almasi, fafanua dhamira ya mwandishi kwa wasomaji wake.

b) Changanua mafunzo yanayopatikana katika riwaya, Ndoto ya Almasi

 

14. Eleza hali ya mazingira anayokabiliana nayo Almasi anapotoka gerezani na uonyeshe anayofanya ili kuyabadlisha.